Kume kuwa na madai na hoja nyingi sana kuhusu hili swala la UTATU. Wengine wanasema kuwa ukijumlisha 1+1+1 unapata 3 na sio MOJA kama ambavyo Wanao amini Utatu wanavyosema.
Tatizo kubwa sio KUJUMLISHA bali unajumlisha kwa kutumia KANUNI ZIPI AU IPI YA HISABATI. Leo katika Max Shimba Ministries tutawajibu watu wote hili swali la HESABU YA 1+1+1 =1? Je, inawezekana au haiwezekani?
HESABU/HISABATI ZINA KANUNI ZAKE NA LAZIMA TUZIFUATE, KWA BAHATI NZURI, hapa Kwenye Huduma yetu ya Max Shimba Ministries tunazifahamu sana KANUNI ZA HISABATI.
Kuhusu swala la UTATU, Linahusisha NAMBA TATU na hivyo sheria yake lazima iwe ya "TERNARY ADDITION" na sio "BASE TEN ADDITION" kama wengi wenu mnao tumia hiyo hesabu bila ya hata kufahamu kuwa addition yenu MNATUMIA SHERIA YA "BASE TEN" .
SASA NINI MAANA YA TERNARY ADDITION:
1. Ternary namba inatumia BASE 3, tofauti na BASE 10 ambayo mkihesabu na kufikia namba 9, unarudi kwenye 1 na kuongeza "SIFURI" = 10. SASA, katika Ternary addition, unapo hesabu namba mwisho wako ni NAMBA MBILI na inayo fuata ni 10, kama kwenye "BINARY ADDITION" namba yako ya mwisho ni MOJA http://www.allaboutcircuits.com/…/d…/chpt-2/binary-addition/ .
1. Ternary namba inatumia BASE 3, tofauti na BASE 10 ambayo mkihesabu na kufikia namba 9, unarudi kwenye 1 na kuongeza "SIFURI" = 10. SASA, katika Ternary addition, unapo hesabu namba mwisho wako ni NAMBA MBILI na inayo fuata ni 10, kama kwenye "BINARY ADDITION" namba yako ya mwisho ni MOJA http://www.allaboutcircuits.com/…/d…/chpt-2/binary-addition/ .
Ninafahamu wengi wenu labda hamjawai soma Hesabu za juu na mnaweza pata walakini, lakini ingia hapa na ujifunze mwenyewe Ternary addition http://homepage.cs.uiowa.edu/~jones/ternary/arith.shtml
SASA TUANZE KUTHIBITISHA UTATU WA MUNGU KWA KUTUMIA HESABU
MSINGI WA TERNARY ADDITION UNATUMIKA:
A. (1 + 1 + 1) Ternary = 10 Ternary
UNAONA JAWABU LAKO NI Ternary (10)
UNAONA JAWABU LAKO NI Ternary (10)
SASA namba zetu tumesha zipunguza na kufikia Tenary 10. Ikiwa na maana kuwa, MSINGI UNAO FUATA NI KUZIJUMLIZA HIZO NAMBA " DIGITS MBILI ZA MOJA NA SIFURI KWA KUTUMIA msingi ule ule wa Ternary addition.
B. (1 + 0) Ternary = 1 Ternary.
SASA TUMESHA PATA JIBU LETU KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA KWA KUTUMIA HISABATI, na leo nimewajibu wale wote ambao HESABU SIO SOMO LAO KUWA UTATU UNAJIBIKA HATA KWA KUTUMIA HISABATI.
SASA NENDA KAMUULIZE MKUFUNZI WAKO WA HISABATI YAFUATAYO:
A. Ternary ya (1 + 1 + 1 ) = ?
B. Ternary ya ( 1 + 2) = ?
B. Ternary ya ( 1 + 2) = ?
UKISHA PEWA JIBU MUULIZE TENA HUYO MKUFUNZI WAKO
C. Ternary ya (1 + 0 ) =?
HAKIKA MUNGU NDIE MWANZILISHI WA HISABATI na hakuna asilo liweza.
Mungu awabariki sana, na leo UMESHA JIBIWA KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA HATA KWENYE HISABATI.
KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA .
A. BABA anaitwa MUNGU ( 1 WAKORINTHO 8:6 ).
B. MWANA ( YESU ) anaitwa MUNGU ( ISAYA 9:6; YOHANA 20:26-29 ).
C. ROHO MTAKATIFU anaitwa MUNGU ( MATENDO 5:3-4 )
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1 na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 21, 2016
April 21, 2016
No comments:
Post a Comment