Saturday, April 21, 2012

Lulu (Elizabeth Michael) Aokoka


Na Sifael Paul
Habari za kuaminika zinadai kuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo ambaye ni mshikiliwa wa kwanza katika kesi ya kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameokoka, Risasi Jumamosi linafunguka.
Kwa mujibu wa mmoja wa waumini 53 wa Kanisa la Efatha Foundation Tanzania lililopo Mwenge, Dar es Salaam linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, Lulu aliombewa na ‘kondoo’ hao wa Mungu wakati akiwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni.
Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa, waumini hao walijikuta wakimwongoza staa huyo sala ya toba huku nao wakiwa na ‘kimeo’ baada ya kufikishwa kituoni hapo wakidaiwa kuhusika kwenye msala wa vurugu na kutaka kubomoa majengo ya kiwanda cha uchapaji cha Afro Plus kilichopo jirani na kanisa lao.
“Ilikuwa Jumatatu ya Pasaka, habari za kifo cha Kanumba zilikuwa zimeshika kasi katika kila kona, tulipopelekwa mahabusu ya Oysterbay ndipo tukamkuta Lulu. Ukweli ni kwamba aliongozwa sala ya toba na waumini akitamka mwenyewe: “Eee Mungu… naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu…
liandike katika kitabu cha uzima wa milele…Ameni.” Alisema mtoa habari huyo.
Wakati huohuo, habari za ndani kutoka lupango Segerea alikowekwa Lulu zilidai kuwa katika siku za karibuni amekuwa kama kachanganyikiwa huku akifanya vitu tofauti ikiwemo kucheza kiduku mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment